Tanzia

Kwa niaba ya Tamasha la ZIFF tungependa kutoa rambirambi zetu kwa ndugu wote waliofiliwa, Waunguja na Wapemba na Watanzania wote kwa ujumla.

Msiba uliotukuta ni mkubwa na umetusononesha vilivyo. Tunaamini sote tumeguswa kwa njia moja au nyingine.

Mwenyezi Mungu Aziweke roho za waliofariki dunia, pema peponi.

Amina